April 14, 2017Kocha Mkuu wa Toto Africans ya jijini Mwanza, Novatus Frugence amedai kuwa wanahitaji kuifunga Simba kwa hali yoyote ili kukwepa kushuka daraja.

Toto ambayo inashika nafasi ya pili kutoka mkiani, itavaana na Simba iliyopo kileleni katika Ligi Kuu Bara, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

“Mechi yetu na Simba tunaichukulia umuhimu mkubwa sana kwani naamini ni miongoni mwa michezo migumu tuliyobakiwa nayo.


“Ushindi utatupa matumaini ya kubaki ligi kuu lakini kufungwa inamaanisha tunajitengenezea uhakika wa kushuka daraja,” alisema Frugence.

Ndani ya kikosi cha Toto African kumekuwa na migogoro inayofukuta, lakini mbaya zaidi kila msimu imekuwa ikipambana kuhakikisha inakwepa kuteremka daraja.


1 COMMENTS:

  1. This time mtatusamehe tu jamanu tuna njaa sana na kombe

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV