April 18, 2017

Kikao cha Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kimeanza kazi yake kujadili rufaa ya Kagera Sugar.

Kikao hicho kinafanyika katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam na uongozi wake umezuia makomandoo wa Yanga na Simba kuingia katika eneo hilo.

Katika kikao cha kamati ya Saa 72 kilichofanyika wiki iliyopita, mashabiki wa soka wakiwemo wa Yanga walijitokeza kwa wingi kwa kuwa kikao kilifanyika katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Kagera Sugar wanapinga Simba kupewa pointi tatu baada ya wao kuwatwanga kwa mabao 2-1.

Simba walipewa pointi tatu baada ya kushindwa, wakidai beki Mohamed Fakhi alicheza mechi yao akiwa na kadi  tatu ya njano.

Simba ikashinda baada ya kamati ya Saa 72 kukaa na kujadili kuhusiana na rufaa yao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV