April 18, 2017

Mmoja wa viongozi wa zamani wa Simba, Chano Almasi aliyekuwa mweka hazina amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Chano anatarajiwa kuzikwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali amethibitisha msiba huo.

“Ni kweli, Chano hatunaye na mazishi ni leo Tandale ambako ndiyo msiba ulipo,” alisema.


Chano alikuwa mmoja wa viongozi katika masuala ya fedha akiwa mhazini msaidizi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV