April 13, 2017Kikosi cha Yanga, kipo tayari kwa safari ya Algeria na maandalizi, kila kitu kipo vizuri.

Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh amesema maandalizi ya safari yako safi kabisa.

“Tuko katika maandalizi ya mwisho, kila kitu kiko vizuri tunashukuru,” alisema.


Yanga inaondoka leo kupitia Dubai kwenda Algers nchini Algeria kuwavaa MC Alger katika mechi ya Kombe la Shirikisho.

Katika mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa, Yanga iliitwanga MC Alger kwa bao 1-0 lililofungwa na Thabani Kamusoko.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV