April 13, 2017



Uongozi wa Mbao FC, umeanza uchunguzi kuangalia kama umehujumiwa katika mechi yake dhidi ya Simba.


Mbao FC ilichapwa kwa mabao 3-2 na Simba katika mechi ambayo ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 82.


Taarifa kutoka ndani ya Mbao FC, zinaeleza kipa Eric Ngwengwe amesimamishwa ili kupisha uchunguzi kwa kuwa ni mtuhumiwa.


Makosa mawili ya kipa huyo yalizaa bao la kwanza na la pili la kusawazisha kwa Simba.


Hata hivyo, taarifa zinaeleza, kipa huyo hajapewa barua ya kusimamishwa zaidi ya kuambiwa kwa mdomo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic