May 17, 2017Serengeti Boys wamesema wake tayari kwa ajili ya mechi yao ya pili ya michuano ya Afcon dhidi ya Angola, kesho.

Hiyo itakuwa ni mechi ya pili ya Boys ambao katika mechi ya kwanza walianza kwa sare ya bila mabao dhidi ya Mali.

Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime amesema wana majeruhi mmoja na wachezaji waliobaki wamejiandaa vya kutosha.

“Kwa kweli tumejiandaa vizuri na tunataka kupata ushindi wetu wa kwanza. Kila mmoja anajua haitakuwa kazi rahisi lakini tutapambana vilivyo,” alisema.


Boys wako katika Kundi B na timu za Mali, Angola na Niger.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV