May 17, 2017



Simba wanatakiwa kushinda zaidi ya mabao nane katika mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu huku wakiomba Yanga ipoteza kwa zaidi ya mabao mawili dhidi ya Mbao FC mjini Mwanza ili wao wawe mabingwa.


Lakini hiyo haiwakatishi Simba tamaa na hawataki kusikia Yanga wakitangazwa kuwa mabingwa kabla ya mechi yao ya mwisho wao wakiwavaa Mwadui FC jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesisitiza bado wanataka kuona matokeo hadi mechi ya mwisho.

“Sisi tunajua bingwa bado hajapatikana na tutaona hadi katika mechi ya mwisho. Tutapambana hadi tone la mwisho.


“Hatuwezi kukata tamaa, huu ni mpira na vijana wako vizuri kabisa,” alisema akionyesha kujiamini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic