May 31, 2017


Kipa mkongwe wa Yanga, Ally Mustapha 'Barthez' na beki wa pembeni wa timu hiyo, Oscar Joshua ni kati ya wachezaji watakaokuwepo kwenye kikosi cha Singida United katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Kama hawatakuwa katika kikosi hicho basi safari yao kwa upande wa Yanga itakuwa imeishia hapo.

Barthez na Joshua ni kati ya wachezaji ambao hawakuwa na nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Mzambia, George Lwandamina katika msimu uliopita wa ligi kuu.
Wachezaji hao wote bado wana mikataba ya mwaka mmoja wa kuichezea Yanga kwenye msimu ujao wa ligi.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani wachezaji hao wataondolewa Yanga na kupelekwa Singida inayofundishwa na Kocha Mkuu Mholanzi, Hans Pluijm aliyekuwa anaifundisha timu hiyo kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na George Lwandamina.

Mtoa taarifa huyo alisema, wachezaji hao walikuwepo kwenye orodha ya wachezaji watakaochwa katika msimu ujao, lakini kutokana na mikataba yao kutomalizika watapelekwa kwa mkopo.

"Barthez na Joshua hawana nafasi ya kucheza katika kikosi cha Lwandamina na pia hana mipango nao, hivyo kama uongozi tumeona tuwatoa kwa mkopo.

"Tutawatoa baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Singida na kukubali kuwachukua, hivyo tumeona tuwaachie waende huko wakacheze,"alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Barthez kuzungumzia hilo alisema kuwa ":Bado sijapata taarifa rasmi ya kupelekwa kwa mkopo, ni tetesi ninazozisikia pekee kama ulivyosikia wewe ni vema tukasubiria kwanza kabla ya mimi kuongea chochote.


"Kingine ni ngumu mimi kuondoka kabla ya kupelekwa huko na Yanga, kama unavyojua bado nina mkataba wa kuichezea Yanga,"alosema Barthez.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic