May 31, 2017


Russia wameingia matatani baada ya kutakiwa kutoa maelezo kutokana na watu wawili aria wa Russia kujichora rangi nyeusi ili waonekane kama Wacameroon.

Watu hao walikuwa katika sherehe za kuitangaza michuano ya Mabara ambayo hufanyika kabla ya Kombe la Dunia.

Mmoja wa watu hao ambaye ni mwanamke, pia alikuwa amejipamba kwa kuvaa ndizi hali inayoashiria dharau au ubaguzi.

Baada ya picha hizo, kumekuwa na mijadala mingi na kwa kuwa Russia ilitakiwa kuwa makini na suala la ubaguzi, tayari suala hilo limezua gumzo zaidi.


Michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 itafanyika Russia ambayo ilishaelezwa kutoa mafunzo kwa watu wake kuhusiana na ubaguzi wa rangi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV