May 25, 2017
John Bocco ni mali ya Simba,. Taarifa zinaeleza amesaini miaka miwili katika kikosi cha Simba.

Taarifa zinaeleza mkataba huo ni wa awali na inaonekana Bocco ameamua kutua Simba baada ya makubaliano yake na Azam baada ya mkataba wake kwisha, kuonekana unakwenda kombo.

Hata hivyo, Bocco amekuwa hapokei simu ili kulithibitisha hilo suala ingawa hivi karibuni alikanusha kila kilichoandikwa kwenye akaunti yake ya Instagram kuhusiana na kwamba ana mpango wa kuondoka Azam.

Alidai akaunti yake ilikuwa imetekwa lakini hali halisi ilionyesha kwamba hakuwa amezungumza lolote.

Afisa Habari wa Azam FC, Jaffar Iddi yeye alisema walikuwa katika mazungumzo na Bocco baada ya mkataba wake kufikia tamati.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV