May 31, 2017



Klabu ya Simba imepanga kuwabakiza wachezaji 15 pekee kati ya 25 iliowasajili msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho (FA).

Timu hiyo, inataka kukiimarisha kikosi chake kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (Caf) watakayoshiriki mwakani.

Wakati wakipanga kusajili na kuwaacha wachezaji hao, tayari baadhi ya nyota muhimu wa Simba wameshaanza kuaga kwenye timu hiyo akiwemo Abdi Banda ambaye mkataba wake umemalizika, wengine ni Jonas Mkude na Ibrahim Ajibu ambao wanaelezwa kuwa wanaweza kuondoka kwenye timu hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, alisema kuwa bado hawajapokea rasmi ripoti ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mcameroon, Joseph Omog lakini tayari Kamati ya Utendaji ilikutana kufanya tathmini ya kikosi chao kwa ajili ya usajili.

Hans Poppe alisema  katika kikao hicho wameona wachezaji kumi ambao hawana mchango na kupanga kuwaondoa katika mipango yao ya msimu ujao wa ligi na michuano ya kimataifa.

Aliongeza kuwa, kati ya wachezaji hao kumi wapo watakaopelekwa kwa mkopo kwa ajili ya kukuza viwango vyao na wengine kuondolewa kabisa.

"Kama ulivyoona msimu huu tulikuwa na kikosi kipana kilicholeta ushindani na kufanikisha malengo yetu lakini licha ya kuukosa ubingwa, kuna kitu tumeonyesha na kufanikiwa kupata Kombe la FA.

"Hivyo basi katika kuhakikisha msimu ujao wa ligi kuu na mashindano ya kimataifa tunakuwa bora zaidi, tumepanga kuwaacha wachezaji 10 kati ya hawa 25 tuliokuwa nao msimu huu.

"Wakati tukiwaacha hao, tumepanga kuongeza idadi ya wachezaji 10 kati yao tunataka wenye uwezo wa kucheza mashindano ya kimataifa, kama unavyojua mwakani tutaiwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo ni lazima tuwe na kikosi imara,” alisema Hans Poppe.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic