May 8, 2017Wakati kesho watakuwa wanaivaa Kagera Sugar, Yanga wamesema hawatajali suala la mechi yao ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar ambayo ilipigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Yanga inaivaa Kagera Sugar kesho katika mechi ya Ligi Kuu Bara ikiwa na kumbukumbu ya kuitwanga vibaya katika mechi ya mzunguko wa kwanza jambo ambalo Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema, hawatalipa kipaumbele na kujisahau.


"Kagera Sugar ni timu yenye uwezo mkubwa na tunatambua ilo kikubwa ni kwamba mchezo wa kesho sio mchezo rahisi na tumejipanga vyema kupambana na Kagera Sugar bila kujali matokeo ya mchezo wa kwanza," alisema.

Katika mechi ya kwanza Yanga iliitwanga Kagera Sugar kwa mabao sita na kubeba pointi zote tatu kwenye Uwanja wa Kaitaba.

"Tuliwafunga mabao sita, lakini sasa tunaendelea kuangalia kuwa tunahitaji pointi tatu muhimu ili kuendelea kupambana kubeba ubingwa," alisema Mwambusi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV