May 8, 2017

Kampuni kubwa ya michezo ya kubahatisha maarufu kama “kubeti” ya SportPesa, inatarajiwa kuzinduliwa nchini rasmi kesho.

Taarifa za uhakika kutoka jijini Dar es Salaam zinaeleza, SportPesa itazinduliwa kesho rasmi.

“Ni kweli tumepewa taarifa kuwa SportPesa wako nchini na uzinduzi rasmi utakuwa kesho Jumanne.

“Tunachukulia kama ni hatua kubwa na jambo jema kwa kuwa tumekuwa tukisikia mara nyingi watu wanashinda huko Kenya mabilioni ya shilingi,” kilieleza chanzo cha uhakika.

SportPesa imekuwa maarufu si kwa ajili ya kubeti tu, lakini ni kampuni ambayo imekuwa ikirejesha fedha inazopata katika jamii.

Nchini Kenya kwa kiasi kikubwa imesaidia kurejea kwa ushindani wa Ligi Kuu ya Kenya baada ya kuidhamini.

Kama haitoshi, SportPesa imewadhamini wakongwe wa soka la Kenya Gor Mahia na AFC Leopards na kusababisha kurudisha kwa ushindani dhidi yao.


Lakini wameendelea kutanua mipaka kwa kudhamini timu kadhaa za Ligi Kuu England kama Hull City, Southampton na Arsenal jambo linalowafanya kwua kampuni hasa ya michezo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV