May 24, 2017Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amechaguliwa kuwa kocha bora wa msimu wa 2016-17 wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Maxime ameibuka na ushindi baada ya kuiwezesha Kagera Sugar kushika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Bara, nafasi ambayo hawakuwahi kuishika kwa zaidi ya misimu sita iliyopita.


Maxime amejiunga na Kagera Sugar akitokea Mtibwa Sugar aliyoitumikia kama mchezaji chipukizi, mkongwe, kocha msaidizi na baadaye kocha mkuu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV