Kipa namba moja wa Azam FC, Aishi Manula ametangazwa kuwa kipa bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2016-17.
Manula amekuwa bora licha ya Azam FC kushika nafasi ya nne mwisho wa msimu kutokana na uwezo aliouonyesha.
Aidha, kiungo mnyumbulifu wa Yanga, Haruna Hakizimana Niyonzima amekuwa mwanasoka bora kwa wachezaji wa kigeni.
Niyonzima raia wa Rwanda aliyeanza msimu vibaya baadaye alibadilika na kuwa msaada mkubwa katika safu ya kiungo ya Yanga ambao wamebeba ubingwa kwa tofauti ya mabao dhidi ya Simba baada ya timu zote kukusanya pointi 68.

0 COMMENTS:
Post a Comment