May 7, 2017Baada ya ukame kumuandama, Mtanzania Mbwana Samatta ameamka baada ya kuifungia timu yake ya KRC Genk bao la ushindi.

Samatta amefunga bao la pili wakati Genk ikiigaragaza Eupen kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Ubelgiji.

Nahodha huyo wa Taifa Stars alifunga bao hilo katika dakika ya 28 baada ya kupokea pasi ya Thomas Buffel, akaupita msitu wa mabeki kwa kasi kabla ya kuukwamisha mpira wavuni.

Kabla ya hapo, Genk ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia Jere Uronen katika dakika ya 18 akiunganisha basi nzuri ya Samatta.Wageni Eupen nao walijitutumua na kupata bao katika dakika ya 76 kupitia Onyekuru.

Kwa ushindi huo, Genk inaendelea kuongoza Kundi B hatua ya play-off ikiwa na pointi 19 na kufuatiwa na Lokeren yenye ponti 10.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV