May 30, 2017Kocha mpya wa Singida United, Hans van der Pluijm, ameendelea na kazi yake ya kukiandaa kikosi chake kipya kwa siku ya pili leo.

Pluijm raia wa Uholanzi, amefanya mazoezi na wachezaji wake kwenye Uwanja wa Uhuru huku sura kadhaa mpya zikionekana pamoja na mshambulizi Atupele Green.

Pamoja na mazoezi, Pluijm alitumia muda mwingi kuzungumza na wachezaji wake akionekana kuwaelekeza mambo mbalimbali ikionekana amelenga kuwajenga kisaikolojia, mapema kabisa. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV