May 30, 2017Kikosi cha timu ya wasichana ya soka ya Shule ya Sekondari ya Makongo, kimeanza kujifua kwa ajili ya kujiweka sawa kwa michuano ya Shule za Sekondari maarufu kama Ummiseta.

Kikosi hicho, leo kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi hayo.

Walianza na mazoezi ya kukimbia ambayo yalionekana kuwa magumu lakini kocha wao alihimiza kuhakikisha wanamaliza.

Baada ya hapo waliendelea na mazoezi mengine ikiwa ni pamoja na "kuupiga" hali inayoonyesha wako vizuri.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV