June 5, 2017


Singida United imeng'olewa katika michuano ya SportPesa Super Cup  baada ya kuchapwa kwa mikwaju 5-4 dhidi ya ACF Leopards ya Kenya.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo. Dakika 90 zilimalizika kwa sare ya mabao 1-1.

AFC Leopards ndiyo waliosawazisha baada ya Singida United inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm kutangulia kufunga bao.

Hata hivyo, Leopards walionekana kuwa na kasi zaidi hasa katika kipindi cha pili kwani pamoja na kupata bao la kusawazisha lakini walitengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV