June 5, 2017


Yanga imetinga nusu fainali ya Sports Pesa Super Cup kwa mikwaju ya penalti.

Yanga imeing'oa Tusker ya Kenya kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila bao.

Kipa wa Yanga, Deo Munishi maarufu kama Dida alichangia kung'olewa kwa Tusker baada ya kupangua moja ya mikwaju ya Wakenya hao.

Sasa Yanga itakutana na Wakenya wengine, safari hii ni AFC Leopards ambao wameing'oa Singida United kwa mikwaju ya penalti pia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV