June 7, 2017


Siku chache baada ya kuondolewa kwenye michuano ya SportPesa Super Cup, Kocha Mkuu wa Singida United Mholanzi, Hans Pluijm amesema kuwa ameona upungufu wa kikosi chake huku akisema atakiboresha kwa kusajili nyota wapya sita.

Kauli hiyo, iliitoa kocha huyo mara baada ya mechi dhidi ya FC Leopard ya michuano hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa Singida kufungwa kwa penalti mabao 4-5 kumalizika.

Mholanzi huyo, juzi ndiyo alianza kibarua cha kukinoa kikosi hicho kwa kukaa kwenye benchi kama kocha mkuu tangu asaini mkataba wa miaka miwili ya kuifundisha timu hiyo.

Pluijm amesema kwa mara ya kwanza amekiona kikosi hicho kikicheza mechi na kuona upungufu kwenye nafasi ya kipa, beki, kiungo na ushambuliaji.

Pluijm alisema, amepanga kukabidhi ripoti hiyo ya usajili kwenye uongozi hivi karibuni kabla ya kwenda kuweka kambi mkoani Mwanza kwa ajili ya kuanza matayarisho ya ligi kuu.

"Tumeondolewa kihalali kabisa kwenye michuano hii mipya ya SportPesa Super Cup, kwa kifupi nimekaa na timu hii kwa muda wa siku sita tangu nimesaini mkataba wa miaka miwili ya kuifundisha na mechi hii ya Leopard ya kwanza mimi kukaa kwenye benchi.


"Kwa kifupi nimebaini baadhi ya upungufu unaohitaji kufanyiwa marekebisho kwa kusajili wachezaji wapya sita wanahitajika kabla ya kwenda kuingia kambini kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu,"alisema Pluijm.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic