June 10, 2017


Mchezaji bora wa mpira wa kikapu kwa sasa LeBron James leo ameingoza timu yake ya Cleveland Cavaliers kushinda kwa pointi 137-116.

Cavs washinde mchezo wao wa kwanza baada ya michezo minne hivyo kufanya matokeo yaws 3-1 katika fainali za NBA.

Awali Cavs walikuwa wamepoteza mechi tatu, mbili ugenini na moja nyumbani na kama wangefungwa leo, safari ingekuwa imewakuta.

Katika mchezo wa leo Cavs walikuwa moto wa kuotea mbali na Kyrie Irving alifunga pointi 40 huku LeBron akionekana kuwa katika kiwango cha juu kabisa.

LeBron alikuwa katika kiwango cha juu zaidi na kuwapa wakati mgumu akina Kevin Durant na Stephen Curry.

Mechi ijayo itachezwa Jumatatu, bado Cavs watatakiwa kushinda ili kuwa salama.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV