June 10, 2017
Klabu ya Azan FC imeendelea kufanya yake baada ya kumsajili kiungo kutoka Mbao FC.

Salmini Hoza ndiye alikuwa akifanya kazi ya ukabaji na kupanga mashambulizi ya Mbao FC na alikuwa akiwaniwa na Yanga lakini tayari amesaini mkataba wa miaka miwili na Azam FC.


Hoza anakuwa mchezaji wa tatu aliyekuwa akitakiwa na Yanga lakini ametua Azam FC.

Awali, Waziri Junior wa Toto African alifika hadi makao makuu ya Yanga na kupiga picha na kombe la ubingwa, mwisho akatua Yanga.

Pili ni Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar ambaye ilibaki kidogo atue Yanga, naye kasajili Azam FC.

1 COMMENTS:

  1. Azam hela wanazo na wanaweza kumchukua yeyote wamtakaye ila ujanja wa mpira na hasa ushindi wa ubingwa, wanasafari ndefu ya kuwashinda YANGA. Subiri uone ligi itakapoanza.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV