June 10, 2017



Msanii Darassa atatumbuiza katika mechi ya fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Darassa ambaye anaendelea kutamba na singo yake ya muziki, tayari amethibitisha kutumbuiza katika fainali hiyo.

“Kweli nitakuwa pale Uhuru kutumbuiza, mashabiki nawakaribisha tupate darasa la burudani ya uhakika ya muziki na soka,” alisema.

Darassa ameahidi kutumbuiza nyimbo zake kadhaa ambazo zinatamba ukiwemo ule mpya.

Fainali ya “Derby ya Mashemeji”, inachezwa kwa mara ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kabla timu hizo, nje ya Kenya zimekutana Sudan na Ethiopia na mara zote Gor Mahia walishinda.


Lakini kesho, mshindi wa fainali hiyo atacheza mechi dhidi ya Everton na kila upande umepania kushinda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic