June 1, 2017Wachezaji wageni watakaofanya kweli katika michuano ya SportPesa Super Cup, wana nafasi ya kuimarisha ushindani ndani ya kikosi cha Simba.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema watatoa nafasi kubwa kwa wachezaji ambao wamesajiliwa au wanaotarajiwa kusajiliwa.

"Michuano ni muhimu sana kwetu, ndiyo maana tutawapa nafasi wageni nao waonyeshe wanastahili kuwa sehemu yetu.

"Unajua wachezaji wetu wamecheza Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho, pia timu ya taifa kwa baadhi, wamechoka. Hivyo watacheza lakini tutawapa nafasi wakati mwingine pia.

"Wageni ambao wamesajiliwa na wale ambao hawajasajiliwa, basi nafasi itakuwa yao," alisema.


Timu nyingine za Tanzania Bara zilizo katika michuano hiyo ni Singida United na Yanga wakati Jang’ombe inatokea Zanzibar.


Timu kutoka Kenya ni Gor Mahia, AFC Leopards na Nakuru All Stars.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV