June 7, 2017Uongozi wa klabu ya Simba hivi sasa upo katika harakati kabambe za kuhakikisha unakisuka upya kikosi chake kwa ajili ya michuano ya Ligi Kuu Bara msimu ujao pamoja na michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika itakayoshiriki hapo mwakani.

Mpaka kufikia sasa uongozi huo wa Simba kupitia kwa mwenyekiti wake wa kamati ya usajili, Zacharia Hans Poppe unadaiwa kufanya mazungumzo na wachezaji mbalimbali wa kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuwasajili ili waweze kuitumikia msimu ujao.

Hans Poppe amesema kwamba, mpaka kufikia sasa wachezaji ambao wameshafanya nao mazungumzo na mambo kuwa sawa anaiona Simba mpya ambayo itakuwa tishio kubwa hapa nchini na anaionea huruma Yanga jinsi watakavyoinyanyasa msimu huo.

Alisema wachezaji ambao mpaka sasa wameshafanya nao mazungumzo ni wa kiwango cha juu na ambao uwezo wao hauna shaka kwa kiongozi pamoja na shabiki yoyote wa Simba.

“Tunaendelea vizuri na harakati zetu za kukisuka upya kikosi chetu kwa ajili ya michuano ya ligi kuu msimu ujao pamoja na ile ya kimataifa ambayo tutashiriki hapo mwakani.

“Hata hivyo mpaka kufikia sasa wachezaji ambao tumeshazungumza nao kuhusiana na usajili ni wa kiwango cha juu sana na endapo tutawasajili hakika hatopona mtu na ninawaonea huruma sana Yanga kwani watapata shida.


“Hata hivyo, kwa sasa siwezi kuwataja majina yao kuwa ni akina nani hao ila tunasubiria kwanza tupate ripoti ya kocha ili  tuone mapendekezo yake na baada ya hapo ndipo tutakapoanza kumalizana na wachezaji hao,” alisema Hans Poppe.

1 COMMENTS:

  1. Ongea saana tu ila utakiona cha moto sie wa Kimataifa Original ni kimya kimya tu!!

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV