June 2, 2017
Bingwa wa Ligi Kuu Bara mwakani atapatikana kwa mfumo wa head to head hasa kama timu zitalingana pointi.

Huo ni mfumo unaotumiwa katika Ligi Kuu Hispania, yaani La Liga na Ligi Kuu Bara ilikuwa inatumia mfumo wa mabao ya kufunga na kufungwa, ile tofauti yaani GD ndiyo iyotoa bingwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameitaka kamati ya utendaji ya shirikisho hilo kupitia upya sheria uwiano wa matokeo timu zilipokutana yaani head to head ikiwezekana itumike katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara kuweza kuamua bingwa wa ligi hiyo iwapo timu zitafungana pointi.


“Kama watafungana kwa pointi tunaangalia head to head, yaani walipokutana, matokeo yao yalikuwaje? Aliyeshinda ndiye anakuwa bingwa,” alisema.

Msimu huu, Yanga wamekuwa mabingwa licha ya kulingana pointi na watani wao Simba kila timu ikipata pointi 68.

1 COMMENTS:

  1. Maana yake kama ingetumika msimu huu simba angekuwa Bingwa kwa point 4-1

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV