June 5, 2017




Sakasaka za usajili kwa timu za Simba na Yanga tayari zimeshaanza kupamba moto na hivi sasa viongozi wa timu hizo wanahangaika kutafuta wachezaji  ili kuviimarisha vikosi vyao kwa ajili ya michuano ya Ligi Kuu Bara msimu ujao pamoja na michuano ya kimataifa.

Kama ilivyo miaka yote inapofika wakati wa usajili timu hizo huonyeshana ubabe pindi zinapogongana kwa mchezaji mmoja na ile ambayo viongozi wake watakuwa wajanja ndiyo ambayo hufanikiwa kumnasa mchezo huo, msimu huu mambo ni hayohayo.
Tayari timu hizo zimegongana kwa beki wa kati wa Mbao FC ya jijini Mwanza, Mrundi, Yusuph Ndikumana ambapo hivi karibuni mchezaji huyo anadaiwa kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ambaye alikuwa nchini Burundi.
Habari kutoka kwa mmoja wa wanaohusika na usajili ndani ya Yanga zimeeleza kuwa baada ya viongozi wa Yanga kusikia hivyo, waliwasiliana na wakala wa mchezaji huyo, Denis Kadito na kumjaza maneno jambo ambalo lilimfanya amtafute Hans Poppe na kuanza kumtolea mapovu, hali ambalo lilimkera sana kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa ndani ya Simba.

Yanga ilifanya hivyo ili Hans Poppe asuse na wao watumie nafasi hiyo kumalizana na beki huyo na inadaiwa kuwa leo wamemtuma mtu nchini Burundi kwa ajili ya kwenda kumalizana na mchezaji huyo.

Kutokana ha hali hiyo, gazeti hili lilimtafuta Hans Poppe ili kujua ni nini kinachoendelea kuhusiana na mchezaji huyo ambapo alidai kuwa hawana tena mpango naye kutokana na kuwa chini ya wakala ambaye ni msumbufu na mwenye manenomaneno mengi yasiyokuwa na tija.

 “Hivi karibuni nilikuwa Burundi kwa kazi zangu, nikiwa huko kuna mtu akanitumia namba ya simu ya Ndikumana akaniambia  mchezaji huyo anataka kuzungumza na mimi kuhusiana na kutaka kujiunga na Simba.

“Nilimpigia simu na nikamuuliza kuwa wewe wakati ukiwa Tanzania watu wa Simba walitaka kuzungumza na wewe lakini ikaonekana una wakala anaitwa Kadito, kwa hiyo nataka unithibitishe kama ndiyo wakala wako au mshavunja naye mkataba.

“Alijibu kuwa bado Kadito ni wakala wake, hivyo nikamwambia basi tuishie hapo kama unamtumia huyo wakala usije kufanya mazungumzo na mimi kwa sababu yeye alitaka kuja hotelini kuzungumza na mimi.


“Hata hivyo baada ya muda Kadito alinitumia ujumbe akinituhumu kwa nini nazungumza na mchezaji wake bila ruhusa yake jambo ambalo lilinishangaza sana,” alisema Hans Poppe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic