June 5, 2017


Timu ya Yanga leo inatarajiwa kushuka uwanjani kuvaana na Tusker FC ya nchini Kenya kwenye michuano mipya ya SportPesa Super Cup, 2017 huku ikitarajia kushusha vifaa vipya vitatu.

Yanga inatarajiwa kuvaana na Tusker majira ya saa 10:15 jioni kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam huku mchezo wa kwanza ukitarajiwa kuanza saa 8:00 mchana utakaowakutanisha Singida Utd na AFC Leopards.

Katika michuano hiyo inashirikisha timu zilizodhaminiwa na SportPesa kutoka hapa nchini Tanzania na Kenya, bingwa wake anatarajiwa kuvaana na Klabu ya Everton ya Uingereza mwezi Julai, mwaka huu.

Meneja Mkuu wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema maandalizi yamekamilika na katika mechi ya kesho wamepanga kuwatumia baadhi ya wachezaji wao wapya waliojiunga na timu hiyo.

Saleh alisema, miongoni mwa wachezaji wapya watakaokuwepo kwenye kikosi hicho ni kiungo mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Mrisho Ngassa, kiungo mkabaji wa Kagera Sugar, Babu Ally Seif na beki mmoja wa pembeni wa Mbao FC ambaye ni sapraizi.

"Kama meneja nimewapokea wachezaji watatu wapya tutakaowatumia kesho (leo) kwenye michuano ya SportPesa Super Cup akiwemo Ngassa na Seif na beki mmoja wa pembeni wa Mbao.

"Pia tutawatumia wachezaji wetu wengine wakongwe na vijana, kama unavyojua nusu ya wachezaji wetu hawapo, wapo kwenye timu zao za taifa," alisema Saleh.

Alipotafutwa Ngassa mwenyewe ambaye alithibitisha hilo kwa kusema: Ni kweli nipo na Yanga kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya SportPesa, baada ya michuano hiyo ndiyo nitajua nini kinaendelea, ingawa bado tupo kwenye mazungumzo.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic