June 3, 2017


Ajabu kabisa inaonekana dunia yote imekuwa against Real Madrid.

Mashabiki wa Madrid leo watakuwa dhidi ya mashabiki wote wa soka ambao wameamua kuishangilia Juventus.

Hamu ya mashabiki wengi isipokuwa wa Madrid pekee, wangependa kuona Juventus inabeba ubingwa wa ligi ya Mabingwa katika fainali ya Uwanja wa Millenium pale Cardiff.

Kila mmoja anaamini Juventus itashinda kwa kuwa ni timu ngumu. Lakini kila mmoja anajua Madrid ni timu hatari sana kwa kufunga mabao mengi. Hili ni kosa kubwa sana kwa kuwa Madrid ina uwezo wa kuivunja kila ngome.

Madrid ina wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kufunga lakini mabeki wawili wa pembeni hatari zaidi na pia viungo wenye uwezo mkubwa wa kutoa pasi za mwisho kama Luka Modric.

Wengi kwa kuwa wanataka Madrid ishindwa, basi wamejiaminisha kuwa safu kali ya Madrid yenye watu wenye njaa kali ya mabao haiwezi kutamba.

Juventus wamecheza mechi 9 za Ligi ya Mabingwa Ulaya bila ya kupoteza lakini katika mechi zote wamefungwa mabao matatu tu.

Wengi wamesahau katika idadi hiyo, Madrid wamefunga mabao 32, hii ni safu bora zaidi ya ushambulizi iliyotoboa kila safu ya ulinzi.


Hii ni mechi ya 50 kwa 50 kwa kuwa safu bora ya ulinzi dhidi ya fowadi kali. Ingawa presha inaonekana ipo juu na inaweza kusababisha kuharibu mchezo kama itatokea kadi nyekundu.


Hii si mechi ya kuhakikisha nani atashinda na nani atafungwa mapema. Badala yake ni suala la umakini kwa kila upande. Ninachoweza kukuhakikishia safu ya ushambulizi ya Madrid hata difensi iwe ngumu vipi, ina uwezo wa kuifunga.

Juventus hawana uwezo wa kuizuia Madrid isifunge bao hata moja kwenye fainali. Kama wanataka wajiandae kufunga mabao matatu, la sivyo hawatakuwa na nafasi kwa kuwa Madird asilimia mia ina uwezo wa kufunga mabao mawili. Wakilala Juventus yanaweza kufika hata manne.


Safu bora ya ulinzi lazima ifanye kazi yake vizuri la sivyo itaadhibiwa lakini safu kali ya ushambulizi lazima itumie nafasi, la sivyo haitakuwa na msaada. Acha sasa twende uwanjani tukaone.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV