June 3, 2017



Na George Mganga
Tathmini yangu kiufupi kuelekea Millenium Stadium, Juventus vs Real Madrid, 3:45 Usiku.

Ni mechi kubwa inayosubiriwa kwa hamu na wapenzi pamoja na mashabiki wote wa mpira duniani.

Timu zote mbili mara nyingi zimekuwa zikitumia aina ya mashambulizi ya kushtukiza, ni #Style ambayo husaidia kuleta matokeo chanya kwa mpinzani endapo tu hakutakuwa na ulinzi imara haswa katika msitari wa mabeki wa mwisho #BackLine.

Juventus wamekuwa na rekodi nzuri ya kuzuia lango lao kuguswa msimu huu na imekuwa timu pekee kuruhusu mabao machache ambayo ni matatu (3) pekee huku timu zote zikicheza michezo sawa (12).

Uchache wa magoli waliyoruhusu Juventus unaonesha kiasi gani sehemu yao ya ulinzi ilivyo imara katika kuhimili mikiki-mikiki ya washambuliaji wa timu pinzani.

Natarajia kumuona Giorgio Chiellin, Leonardo Bonucci na hata Andrea Barzagli katika ulinzi wakiidhibiti vizuri #Combination ya #BBC (Bale, Benzema na Cristiano) iliyofunga mabao 32 katika mechi 12 za msimu huu #UCL.

Licha ya kuwa na mabao mengi ya kufunga, #BBC inaingia ikiwa na udhaifu kwa upande wa Gareth Bale ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeraha msimu huu na sidhani kama anastahili kupata nafasi ya kuanza.

Uwepo wa Dan Alves katika winga ya kulia unatoa nafasi ya kuwatengenezea wenzake krosi safi katika #StrikingForce ya Juventus. Alves mzuri zaidi katika upikaji wa mipira hiyo, hivyo sitaraji kuona akishindwa kuwalisha wakina Higuain, Dybala 'Messi Mpya :)' na hata Mandzukic katika nafasi ya umaliziaji.

Achilia mbali kuachwa kwao kwa mataji na Madrid waliolitwaa mara 11 huku Juve akilibeba mara 2 pekee, naamini watafanya kila jitihada kuhakikisha wanalibeba taji hili chini ya Kocha Massimiliano Allegri ambaye hawatopenda kumuangusha ili wafikishe mataji matatu.

Nategemea kuiona Juventus ikitumia mfumo wa 4-2-3-1 kama walioutumia dhidi ya Barcelona ambayo waliinyima nafasi ya kucheka na nyavu kwa dakika 180 na kuwaondoa mashindanoni.

Mfumo huu utasaidia zaidi kuwanyima uhuru Madrid ya kutengeneza #Patterns haswa katika eneo la kati ambalo atakuwepo Ton Kroos, Casemiro na hata Luca Modric kutegemeana na ubora utakaokuwepo kwa Juventus na pande zote mbili.

Kuelekea mechi hii natagemea kuona mfumo wa 4-3-1-2 kwa Real Madrid ambao pia ni wa kujilinda zaidi ili kuwabana Juventus kutengeneza mianya ya kufanya #CounterAttacking.

Hii ni tathimini yangu tu, dakika 90 siku zote huwa zinakuwa mwamuzi wa mwisho.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic