June 30, 2017


Makamu Rais wa TFF, Wallace Karia amewekewa pingamizi kwa kuwa ni raia wa Somalia.

Karia anagombea nafasi ya Rais wa TFF katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma.

“Kweli nimewekewa pingamizi na mtu anayesema mimi raia wa Somalia jambo ambalo si kweli. Baba yangu mzazi ni mzaliwa wa Somalia lakini mimi ni Mtanzania.

“Nimetoa kila kitu changu lakini baadaye wamesema watafuatilia uhamiaji,” alisema.


Karia amesisitiza baada ya kubainika ukweli basi angependa aliyeweka pingamizi afikishwe katika kamati ya maandalizi kwa kusema uongo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV