Nakuru All Stars imekuwa timu ya tatu ya Kenya kutinga nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup.
Nakuru imeitwanga Simba kwa mikwaju ya penalti 5-4 na kutinga nusu fainali na sasa itacheza na Gor Mahia ya Kenya pia.
Dakika 90 kati ya Nakuru na Simba iliisha kwa sare ya bila bao huku Nakuru wakionekana kupoteza nafasi nyingi zaidi.
Simba ilipewa nafasi ya kusonga kwa kuwa ni wazoefu na Nakuru si timu kubwa.
Simba iliwajaribu wachezaji kadhaa wakiwemo kutoka Rwanda lakini haikuonyesha makali sana.
Wakati wa upigaji penalti, wachezaji wawili wa kimataifa wa Simba, kipa Daniel Agyei ndiye aliyekosa penalti hiyo moja huku yeye akiruhusu zote tano kutinga wavuni.
0 COMMENTS:
Post a Comment