June 6, 2017



Mmoja wa viongozi mahiri waliokuwa wakihusika na masuala ya usajili wakati wakiongoza klabu ya Yanga, Seif Ahmed “Magari” amesema hahusiki na usajili kwa kuwa kwa sasa si kiongozi wa klabu hiyo.

Magari amesema yeye na swahiba wake Abdallah Bin Kleb wamesikitishwa na kitendo cha wao kuhusishwa na usajili wa klabu hiyo wakati hawajui lolote.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Seif Magari amesema:

“Unajua pale Yanga kuna viongozi, ukizungumzia kamati ya usajili au ufundi ipo na imeteuliwa kwa kufuata utaratibu sahihi.

“Sasa nashangaa kuona kwenye vyombo vya habari. Hata Abdallah (Bin Kleb), naye ni kama mimi, anashangazwa na hilo.

“Ushauri wangu watu wasitumie majina yetu vibaya. Kwangu mimi ni mwanachama wa Yanga, nitaendelea kubaki hivyo lakini usajili tuwaachie viongozi wafanye kazi yao kwa kuwa tunawaamini. Hatujui lolote kuhusiana na usajili,” alisema.

Hivi karibuni, imekuwa ikielezwa wawili hao ndiyo wanaosimamia usajili wa Yanga hasa baada ya aliyekuwa Mwenyekiti, Yusuf Manji kubwaga manyanga.

Magari na Bin Kleb wanajulikana kwa umahiri wao wanaposhiriki katika zoezi la usajili na wao ndiyo walishiriki katika zoezi la kumnasa Kelvin Yondani kutoka Simba, jambo ambalo lilionyesha kuwakera Msimbazi hadi leo.


2 COMMENTS:

  1. Kama kweli Seif Magari na Bin Kleb wana mapenzi na Yanga (Hata kwa wale wengine waliokuwa wakidai Manji Atuachie Yanga yetu) naamini huu ni wakati muafaka wa kuingia mzigoni kuiokoa Club kwani hali si nzuri financially!!, MATENDO HUKIDHI HAJA MARIDHAWA KULIKO MANENO.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahaha....Wanasubiri mpunga wa sport pesa maana wana uhakika mkate upo na utagawanwa

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic