June 3, 2017
DAR ES SALAAM, JUNI 2, 2017. Tiketi za michuano ya SportPesa Super Cup inayotarajiwa kuanza tarehe 5 Juni 2017, zimeanza kuuzwa rasmi kuanzia tarehe 1 Juni kupitia Kampuni ya Selcom ambapo bei za tiketi za VIP ni 15,000/- na 10,000/- wakati bei za tiketi za kawaida ni 3,000/- tu.

Wananchi wenye kadi za Selcom wameanza kupata kadi za mechi hizo na wengine wanaweza kununua tiketi za mechi husika kuanzia saa tatu kamili asubuhi uwanja wa Uhuru. SportPesa na Selcom inawatangazia wapenzi wa soka kununua kadi za Selcom kwa muuzaji aliyepo karibu yao.

Michuno ya SportPesa Super Cup itafanyika katika uwanja wa Uhuru uliopo pembezoni mwa Uwanja wa Taifa, ambapo itazikutanisha timu 4 kutoka Tanzania na timu 4 kutoka Kenya katika kuwania kitita cha Dola za kimarekani elfu thelathini (US $ 30,000)   na mshindi wa fainali hizo atapata nafasi ya kuvaana na timu ya Everton kutoka Ligi kuu ya England mwezi Julai tarehe 13.

Wapenzi wa soka wanaweza kununua tiketi za mechi kupitia simu zao za mkononi kwa kufuata hatua zifuatazo: 

  1. 1. Kwa wateja wenye kadi za Selcom bofya *150*50#, andika namba ya kadi yako ya Selcom, kisha chagua namba 3 ambayo ni burudani /Michezo.
  2. 2. Weka pesa kwenye kadi kupitia wakala au duka la Selcom, au kupitia kadi nyingine ya Selcom. 
  3. 3. Wateja wanaotumia mtandao wa Airtel wanaweza kuweka pesa kwenye kadi zao kupitia Airtel Money kwenda namba ya biashara 172255. 
  4. 4. Kwa wateja wanaotumia huduma za benki kwa njia ya simu (Mobile Banking) wanaweza kuweka pesa kwenye kadi zao za Selcom kupitia Akiba Commercial bank, Exim Bank, Mkombozi Bank na Stanbic Bank au kwa kutembelea tawi lolote la Akiba Bank na NMB Bank na kujaza kadi moja kwa moja.

Michuano ya SportPesa Super Cup itaanza kwa AFC Leopards ya Kenya kuchuana na Singida United huku mabingwa wa Vodacom Premier League Yanga SC wakichuana na mabingwa wa SportPesa Premier League Tusker FC ya Kenya siku ya tarehe 6.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV