June 8, 2017



Katika timu nne zilizoingia nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup, mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga ndiyo tumaini pekee la Watanzania.

Yanga imetinga hatua hiyo baada ya kuing’oa Tusker kwa mikwaju ya penalti na leo itashuka dimbani saa 8 mchana kuwavaa AFC Leopards ya Kenya.

Yanga inataka kushinda ili kutinga fainali ya michuano hiyo kwa kuwamaliza Leopards lakini nao wanaitaka nafasi hiyo.

Mechi ya Yanga inasubiriwa kwa hamu kwa kuwa ndiyo timu pekee ya Tanzania ambayo imebaki katika michuano hiyo.

Iwapo Yanga itatolewa leo, maana yake uhakika asilimia mia kuwa timu ya Kenya ndiyo itakayocheza mechi ya kirafiki dhidi ya na Everton Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baada ya mechi hiyo kati ya Yanga dhidi ya Leopards, Saa 10 jioni kutakuwa na mechi kati ya Gor Mahia dhidi ya Nakuru All Stars walioing’oa Simba mashindanoni kwa mikwaju ya penalti.

Tayari Kenya ina uhakika wa kupeleka timu moja nusu fainali hasa kupitia mechi kati ya Gor dhidi ya Nakuru.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic