June 9, 2017






Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limetangaza wamuzi wa mchezo kati ya Tanzania na Lesotho unaotarajiwa kufanyika Jumamosi Juni 10, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa CAF, waamuzi hao ni Abdillah Mahamoud - atakayekuwa mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Gamaladen Abdi na Farhan Bogoreth wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Twagirumukiza Abdoulkarim kutoka Rwanda huku Kamishna akiwa ni Amir Hassan wa Somalia

Waamuzi hao pamoja na kamishna wanatarajiwa kufika Dar es Salaam, Tanzania kesho Ijumaa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) wakati wapinzani wa Taifa Stars wanaingia jioni ya saa 11.55 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini. Timu hiyo itafikia Hoteli ya Southern Sun, Dar es Salaam.

Mchezo kati ya Taifa Stars na Lesotho, utafanyika kuanzia saa 2.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam uliko Chamazi, Dar es Salaam na ili kuwapa fursa Watanzania wengi kushuhudia mchezo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeondoka kiingilio cha Sh 15,000.

Hivyo sasa Viingilio katika mchezo huo vitakuwa ni Sh 10,000 kwa Jukwaa Kuu wakati mzunguko itakuwa ni Sh 5,000.

Kujiandaa na Mchezo huo Taifa Stars ilipiga kambi hapa nchini kuanzia Mei 23, mwaka huu kabla ya kwenda Alexandria, Kaskazini kabisa mwa nchi ya Misri ambako ilipiga kambi ya wiki. Kambi hiyo ilifurahiwa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga.

Mchezo huo dhidi ya Lesotho utakuwa ni wa kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi ‘L’ kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika Cameroon.


Mbali ya Lesotho na Tanzania, mataifa mengine katika Kundi ‘L’ ni Uganda na Cape Verde ambao pia wikiendi ya Juni 9, 10 na 11, mwaka huu watakuwa katika mchezo wa kwanza pia kuwania nafasi hiyo. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic