Kiungo Haruna Niyonzima ni kati ya wachezaji ambao wanamaliza mkataba wao na Yanga baada ya siku kadhaa.
Hali hiyo imefanya awe anahusishwa na kujiunga na timu kadhaa na hasa watani wa Yanga, Simba.
Hii imekuwa kila unapokaribia usajili mpya lakini safari hii, Niyonzima mwenye ameamua kuelezea kuhusiana na hilo na kama kweli amenuia kujiunga na Simba au kubaki Jangwani.
"Hizo ni tetesi za usajili, siwezi kukuficha kitu chochote bado sijafanya mazungumzo na Simba, mimi bado mchezaji halali wa Yanga.
"Mkataba wangu unatarajiwa kumalizika mwezi ujao na mara baada ya kumalizika nitawapa nafasi kwanza klabu yangu ninayoichezea kabla ya kuchukua maamuzi mengine ya kusaini timu nyingine, mimi nipo Rwanda na mara nitaporudi nitakutafuta (mwandishi) kwa ajili ya kukuelezea kwa undani."
0 COMMENTS:
Post a Comment