Arsenal imetangaza usajili wa beki wa Schalke Sead Kolasinac raia wa Bosnia.
Kocha Arsene Wenger anaonekana kuanza mambo mapema kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake na beki huyo wa kushoto alikuwa huru.
Awali timu kadhaa zilikuwa zikimuwania Kolasinac wakiwemo mabingwa wa England, Chelsea.
Timu nyingine ambazo zilionyesha nia ya kumpata kabla ya Wenger kuchangamka ni pamoja na Manchester City, Liverpool, Everton, Juventus na AC Milan.
0 COMMENTS:
Post a Comment