July 5, 2017Baada ya kumkosa Donald Ngoma ambaye ilikubaliana naye kila kitu, Simba iko katika hatua za mwisho kumsajili mshambulizi kutoka nchini Ghana.

Kuna taarifa tayari Simba imefanya mazungumzo na mshambuliaji huyo ikimtumia mmoja wa viongozi wake.

Hata hivyo Simba wamekuwa wakifanya siri kubwa kuhusiana na mshambuliaji huyo hasa jina na timu anayotokea kwa hofu kuwa kuna timu zinaweza kuwawahi na kumsajili.


Imeelezwa kiongozi wake aliyekwenda Ghana na kufanya mazungumzo ya awali na mshambuliaji huyo ni Abbas Ally ambaye ni mratibu wa Simba.

"Abbas alikuwa Ghana ambako alizungumza na mshambulliaji huyo pamoja na kuhudhuria harusi ya Kotei," kilieleza chanzo.

"Kwanza alianza kwenda mazoezi, alimuona na amechukua clip za baadhi ya mechi zake na pia mazoezini. Tayari watu wa kamati za usajili na ufundi, wanaonekana kumkubali."

Juhudi za kumsaka Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe maarufu kama ZHP zinaendelea.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV