July 6, 2017Wakili aliyekuwa akimtetea Rais wa TFF, Jamal Malinzi, amejiondoa.

Jerome Msemwa amejiondoa kumtetea Malinzi ambaye anakabiliwa na mashitaka 25 yakiwemo ya matumizi mabaya ya ofisi na utakatishaji fedha.

Taarifa zimeeleza, Msemwa amejitoa kutokana na kutopata maelezo kutoka kwa mteja wake.

Kujiondoa kwa Msemwa, maana yake amebaki Alloyce Komba ambaye alikuwa pamoja na Msemwa.


Hadi sasa, Malinzi pamoja na katibu wa TFF, Mwesigwa Celestine na mhasibu wa shirikisho hilo wako mahabusu wakisubiri kurejea mahakamani Julai 17, kesi hiyo itakaposomwa tena.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV