July 5, 2017


Mshahara wa pauni 230,000 (zaidi ya Sh milioni 659) kwa wiki wa Wayne Rooney umeonekana kuwa sehemu ya kikwazo kwake kurejea Everton.

Tokea jana imekuwa ikielezwa, Rooney amechukua uamuzi wa kuachana na kwenda China au Marekani na badala yake kurejea Everton aliyojiunga nayo akitokea Man United.

Everton imeitaka Man United kushirikiana nayo kulipa mshahara huo itakapomchukua Rooney kwa mkopo wa muda mrefu.

Lakini kama itamnunua, bass itabidi iuziwe kwa kiwango cha chino kwa ajili ya kuweka fungi la mshahara.


Hata hivyo, imeelezwa pande hizo tatu yaani Man United, Everton na Rooney watalazimika kukaa pamoja ili kulimaliza suala hilo na masuala mengine ambayo yatamuwezesha Rooney kurejea Everton ambayo itakuja nchini kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa SportPesa Super Cup, Gor Mahia Agosti 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV