July 22, 2017



Deus Kaseke amemalizana na Singida United na mara moja amepaa kwenda Mwanza kuungana na wenzake.

Kaseke aliamua kutua Singida United baada ya kushindwa kumalizana na viongozi wa Yanga katika suala la maslahi baada ya mkataba wake kwisha mwishoni mwa msimu uliopita.

Kiungo huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu, anatua Singida United na kuungana na kipa Mustapha Ally Barthez waliokuwa pamoja Yanga ambaye amejiunga juzi na matajiri hao wa kanda ya kati.

Pamoja na Barthez, Kaseke anaungana na kocha wake wa zamani, Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic