September 23, 2018


Na George Mganga

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano katika klabu ya Yanga, Hussein Nyika, amesema kikosi chao kipo tayari kwa mchezo wa leo dhidi ya Singida United.

Yanga itakuwa ina kibarua kizito mbele ya Singida majira ya saa 1 jioni ikiwa imetoka kujeruhiwa na African Lyon kwa kufungwa mabao 3-2.

Nyika amesema wao wanatambua kuwa Singida ilitoka kufungwa na Lyon lakini watapigana kulingana na namba Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera alivyowaandaa wachezaji wake.

Aidha, Nyika amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi katika mchezo dhidi ya watani zao wa jadi Simba utakaopigwa Septemba 30 2018.

Nyika ameeleza ujio wa mashabiki na wanachama wengi kwa wingi uwanjani utachangia kuwadhoofisha Simba kwa sababu hamasa itakuwa kubwa ndani ya Uwanja.

"Ni vema mashabiki na wanachama wetu wakaja kwa wingi zaidi kwenye mechi yetu na Simba, leo tunamalizana na Singida kisha tutajiandaa kukabiliana na Simba Septemba 30" alisema.

7 COMMENTS:

 1. Waende hao wasioijua simba , mimi sithubutu kwani mnyama huwa anatisha tukikutana nae

  ReplyDelete
 2. Mpira hauna historia .Muulize Mourinho.

  ReplyDelete
 3. Simba yenyewe imetepeta iko hoi Yanga nendeni tuu mkajipigie sisi wa simba hatutaenda wataenda viongozi na Aussems. Hatupendi aibu ss!!

  ReplyDelete
 4. Kwa Simba hii inayosemewa na viongozi wake, mocha msaidizi Djuma sio muhimu, mpira una matokeo matatu, hawataki ushauri wa mashabiki wake, sijui kwakweli. Naipenda Simba lakini , mahusiano ya makocha yanaharibu timu na viongozi wanatafuta visingizio badala ya muleta umoja kwa walimu wa timu.

  ReplyDelete
 5. Kwa Simba hii inayosemewa na viongozi wake, kocha msaidizi Djuma sio muhimu, mpira una matokeo matatu, hawataki ushauri wa mashabiki wake, sijui kwakweli. Naipenda Simba lakini , mahusiano ya makocha yanaharibu timu na viongozi wanatafuta visingizio badala ya muleta umoja kwa walimu wa timu.

  ReplyDelete
 6. Mechi za timu hizi mbili huwa hazitabiriki
  Msitumie kigezo cha mmoja kuwa dhoofu kwa wakati huu kama kipimo cha kufungwa au kutofungwa kwa mmoja wao inagawa ni viashiria vya matokeo. Kwa wakati huu Yanga imeendelea kuimarika lakini pia siyo kipimo cha kumfunga mtani wake. Wapenzi wa pande mbili wajitokeze kwa wingi kuiona game hii muhimu ambayo pia huchukuliwa kuwa kipimo cha wachezaji na makocha.

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV