September 23, 2018


Na George Mganga

Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ameshikwa na homa ya tumbo ambalo limempa wakati mgumu kwa siku mbili sasa.

Manara ambaye alikuwa Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Simba dhidi ya Mbao, ameeleza kuwa tayari ameshaelekea hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi.

Licha ya kutumia dawa kwa ajili ya kukata maumivu, Manara amesema kuwa dawa hizo hazijasaidia chochote kile na imembidi aelekee hospitalini kwa ajili ya vipimo.

"Dua zenu aumwa sana, ninapelekwa hospitali maana hali si shwari, tumbo linasokota kwa siku mbili sasa na dawa zimeshindwa kufanya kazi" amesema Manara.

Wakati Manara akisumbuliwa na tumbo, timu ya Simba ipo mjini Shinyanga hii leo kucheza na Mwadui FC ikiwa ni mechi ya Ligi Kuu Bara majira ya saa 10 kamili jioni.

6 COMMENTS:

  1. Kuwa makini usije kuhara dam jioni ya leo

    ReplyDelete
  2. Upumbavu mtupu. Binadamu mwenzako anaumwa mtu mzima hovyo unaombea azidi kuumwa.Ujinga pia una mipaka. Badilika .

    ReplyDelete
  3. Mungu atampa nafuu InshaAllah. Maumivu sugu ya tumbo mara nyingi huwa ni dalili ya uwepo wa matatizo mengine makubwa zaidi ndani ya mwili. Kula chakula chenye maumbukizi hasa mboga mbichi zilizoandiwa kwa ajili ya saladi mfano cabbage mara nyingi hubeba bacteria ambao hawatibiki kirahisi mpaka kwa dawa maulum. Wakati mwengine maumivu sugu ya tumbo husababishwa pia na hali ya mabadiliko ya mwenendo wa kawaida ya mishipa ya kusukumia chakula tumboni kuwa dhaifu, kwa kisukuma wanaita (Gastroparesis). Kuna vitu vingi vinaweza kuchangia(gastroparesis) mfano utumiaji wa dawa za maumivu,utumuaji wa baadhi ya dawa za kuondosha mawazo,blood pressure nk.
    Dalili kama maumivu ya tumbo yanayoambatana na tumbo kujaa gesi na kutopata choo kilicho sawa au wakati mwengine hata kujamba kwa shida,kupata maumivu ya tumbo mara tu baada ya kula,kuhisi kutapika yaani kichefuchefu na hata kutapika,kukosa hamu ya kula ni baadhi tu kati ya dalili kadhaa ya gastroparesis. Kwa wagonjwa wenye kisukari hali inaweza kuwa mbaya zaidi. Mgonjwa anashauriwa kuacha kula vyakula vibichi kama vile mboga mboga na matunda na kutakiwa kula vyakula vilivyopikwa na kuiva sawa sawa mfano wali mweupe na mayai ya kuchemsha. Viazi mviringo na vitamu na kujiepusha na vinywaji vya soda na vile vyenye asili ya acid. Cha msingi ni mgonjwa kujiepusha na vyakula ambavyo vitaifanya hali yake kuwa tete zaidi, wataalamu wa afya wanaelewa zaidi ila kusaidiana mawazo ni kitu cha msingi zaidi kiliko kukaa kimya au kuleta kejeli kunako maradhi.

    ReplyDelete
  4. mungu akuponye haraka mtani urudi kwenye majukumu yako,kwani ni raha sana simba ikifungwa na wewe uwepo ili utuletee habari sahihi

    ReplyDelete
  5. mechi tar.30 we unaanza kujiharishia hovyo leo

    ReplyDelete
  6. mechi tar.30 we unaanza kujiharishia hovyo leo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic