Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Samuel Lukumay ameshangazwa na baadhi ya wanachama na mashabiki wa klabu yao juu ya kumshutumu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hussein Nyika kuhusiana na usajili.
Lukumay amesema baadhi yao wamefikia hatua ya kusema Nyika alimdanganya Kocha Zahera kuwa alimwahidi baadhi ya wachezaji lakini mwisho wa siku ikawa si kweli kama walivyokubaliana.
Kaimu Lukumay ameeleza ifikie hatua wapenzi wa Yanga waelewe klabu yao inapitia wakati gani hivi sasa kwani baadhi ya wachezaji aliowapendekeza Zahera dili zao zilikuwa kubwa na kuepelekea kushindwa kuwasajili.
Kiongozi huyo aliyekaimu nafasi hiyo kwa muda, ameshangazwa na lawama nyingi za wanayanga ambao hawajui klabu ipo kwenye hali mbaya kiuchumi kipindi hiki.
Yanga imefanikisha kunyaka saini mbili pekee za wachezaji katika dirisha ambao ni kipa Ibrahim Hamid na aliyewahi kuwa mchezaji wa Simba, Haruna Moshi 'Boban'.
Kwa wasomaji wa Blog yetu pendwa ya michezo hakikisha una nifollow INSTAGRAM kwa kubonyeza link iliyopo hapo Juu tutakudodoshea Upates zote za michezo kuanzia sasa.
Asante
BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS
Hakuna anayekataa kuwa klabu yenu ina pita kwenye kipindi kigumu cha uchumi lakini kinachoongelewa hapa ni kauli za uongo za Nyika na kamati yake kumdanganya kocha kwa nini asimwambie wazi kama uwezo wa kusajili hatuna kuliko kumdanganya kama kila kitu tayari na wachezaji tumeshamalizana nao,sasa sijui wewe unajaribu kuongea kitu gani ili tukuelewe uongo haufai ilikuwa muweke wazi kama hatuna uwezo wa kuongeza mchezaji sio kusema uongo hata wewe unaonekana una tatizo fulani katika kichwa usijaribu kumkingia kifua Nyika ni siku chache tu zimepita amesema hakuna mtu yeyote wa kumwingilia kwenye majukumu yake, kama kocha anaweza kuondoka kwani sio muhimu sana kwenye timu yenu mna makocha wengi wameomba kazi hapo Yeye Zahera han umuhimu wowote ule.
ReplyDeleteYour very clever brother! that what i thought too and what Nyika should do, He should be clear and then both side could be understanding. But he did not showing inventiveness or originality to answer after coach telling him the truth cuz of the way i felt after window be closed. Nyika he must go cuz he is very rude and enginorent stupidly. Na anaongea kama yeye timu ni yake kama alivyo Zambunda na Lyon yke really? who is Nyika???
Deleteumenena vema broo.
DeleteHuyo Lukumay nae ndiyo wale wale kichwa pumba sijuhi watu kama hawa wanatoka wapi njaa tu. seriously>
ReplyDeleteHonesty and truth are the first chapter in the book of wisdom
ReplyDeleteLukumay tunamfukuza muda si mrefu...nae anataka kutuongopea
ReplyDeleteWote wapigaji wa hela hao, mchezaji anasema milion kumi wao wanahitaj milion 20 kutoka kwenye club ili hela inayozid waile
ReplyDeleteMbona staiker wa mwadui alsema mil 10, alafu nyika akaidai club mil 20...? Hzo kumi alizoongeza zilikuwa za nn...?
VIONGOZI WENGI YANGA NI MAUMBWAA
Wanadai team haina pesa jiulze hivi
KWANINI VIONGOZ HAWAJAWAH KUGOMA KWA KUSHINIKIZA MISHAHARA...?
Wwanasema club haina hela MBONA MISHAHARA YAO WANAJIINGIZIA...?
Club ya yanga hela ipo hata ya usajili ipo ila KUNA WATU WAMEMUWEKA NYIKA ili wawe wanaiibia yanga hela HASA KWENYE USAJILI
Kila mchezaj wanapiga cha juuu
NDIO MAANA WANAKATAA UCHAGUZ WANAJUA WATATOLEWA
kaka mbona unapunguza dau!!!!!! hakusema 20.....nyika alisema 25
ReplyDeleteKwa nn wamdanganye???!
ReplyDeleteLukumai shika adabu yako na kauli zako wanayanga tuna akili timamu, ukimtetea Nyika basi nawe ni mwizi unaweza kutuachia Yanga Yetu vilevile, hata tukikubaini mwizi itakulakwako, tunakuheshimu sana
ReplyDelete