September 5, 2019


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa halitakuwa na huruma kwa klabu yoyote itakayotaka kubadili rangi ya nembo ya wadhamini wao kwa msimu huu wa 2019/20 katika Ligi Kuu Bara.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Rais wa TFF kupitia Rais wake, Wallace Karia, kuingia mkataba mwingine wa udhamini na benki ya KCB.

Karia amesema hivyo akieleza wadhamini wanapaswa kuheshimiwa hivyo haitaruhusiwa timu yoyote ile kuvaa jezi ambazo hazina nembo yenye rangi rasmi ya mdhamini.

Aidha, Karia amesema kuwa kwa baadhi ya makocha wanaoingia uwanjani na jezi zenye nembo ya makampuni mengine tofauti na za wadhamini wanaotambulika na TFF lazima wawachukulie hatua.

Kauli hii inakuwa inazidi kuleta wakati mgumu kwa Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ambaye amekuwa akivaa tisheti zenye nembo ya POLO sambamba na klabu yake ambayo inaelezwa imegomea kuvaa jezi zenye nembo nyekudu kutoka Vodacom.

18 COMMENTS:

  1. Karia zungumza na viongozi was timu husika sio mnakimbilia magazetini

    ReplyDelete
  2. Ndugu yangu wewe ni mmoja kati ya viongozi waliofeli vibaya katika uongozi wako na majukumu yako ya kila siku,hii inaonyesha wazi huna upeo wa kuongoza hata kata wacha chama cha mpira cha Wilaya,ni ujinga mkubwa sana unao ufanya baada ya kuandaa mikutano na watendaji wa vilabu unakimbilia magazetini na kwenye vyombo vya habarikutisha vilabu kwa kweli kijana huna jipya kabisa subiri muda wako uishe tuangalie utakapoangukia wenzio wameangukia mahakamani sijui wewe?

    ReplyDelete
  3. Hebu fanyeni mambo ya msingi acheni malumbano yasiyo na tija na afya katika maendeleo ya soka....visasi na chuki katika soka havina mahala pake katika tasnia ya soka...mambo kama uboreshwaji wa miundo mbinu kama viwanja na kuwaongezea ujuzi waamuzi na makocha wazawa hayo ndiyo mambo ambayo TFF na Bodi ya Ligi Inatakiwa kuyafanya na vyombo vya habari ikiwamo blogu hii ya Salehe jembe msichochee malumbano na mijadala kama hii

    ReplyDelete
  4. Ubabe utakuumizeni. Mbona timu nyengine zote hatuzisikii kuzozana na TFF, wachezaji wala marefa. Imefika wakati mjipime na kujisahihisha. Wapeni nafasi viongozi WA Mpira kuyafanya yenye masilsha

    ReplyDelete
  5. TFF upande mwingine mko sawa na upande fulani mnafeli. Timu za Tanzania hazitegemei wadhamini wa ligi tu kuna wadhamini wengine. Kaeni na viongozi mjadili namna ya kuboresha hilo.

    ReplyDelete
  6. Kuna timu ya kulalamika tu.Hata sheria za mpira wanataka zibadilishwe.Nembo ikiwa na rangi tofauti inakera nini.Simba walivaa nembo ya njano ya CAF ulisikia kelele?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sidhani lawama zimetolewa officially na Yanga ni hisia tu za vyombo vya habari kuhusu nembo ya vodacom kuwa na rangi tofauti na asili ya Yanga kwa hiyo inahisiwa kuwa Yanga watapinga lakini hakuna mahali wametoa kauli ya kupinga au kukubali ila ni uchochezi unaoendelea kufanywa na vyombo vyetu vya habari

      Delete
  7. Wacha mwenyekiti TFF afanye hivyo kwa sababu anapofanya akaona upande wa pili umefurahi anaona atafute jingine la kuumiza Yanga. Lakini haya yote yana mwisho hata kwenye vitabu vya dini Herode alipoona kuwa akiwaua wanafunzi wa Yesu Wayahudi walifurahi akatafuta kumwua na Petro lakini Mungu akamtoa kifungoni. Tunajua Mungu atuwapa Yanga njia ya kutokea kwenye haya yote yanayotoka TFF.

    ReplyDelete
  8. watu wa yanga kwa kulalamika acheni kudeka

    ReplyDelete
  9. Unaweza mwona mtu mwenyewe ni mwekundu kila saa akitaka support ya wekundu. Lakini undani wa kila kinachoendelea hauwezi kuwa wa muda mrefu utajulikana.

    ReplyDelete
  10. Log ya voda?????. Mtaishia kutembeza bakuli ninyi ombaomba fc

    ReplyDelete
  11. Yaan huyu anazunguka tu maneno yake uko kote kama kaweka pazia tu ila lengo kuu anaiongwlea yanga kwen aseme hvyo aliona yanga kuwa na rangi tofaut na mantik yake au. Ila sio mbaya kutumia uongoz wake kuwakandamiza timu nyingine walikuwepo na wengi na watakuwa wengne baada yako tuone ukae milele kwenye uongoz wako kenge ww

    ReplyDelete
    Replies
    1. hahaaahaaa kama Malinzi alivyoondoka TFF au unajifanya umesahau.Sindano inawaingia eeh

      Delete
  12. Safi karia shikilia msimamo wako watu wanamsifia zahera wakati hata nguo zenyewe anavaa hovyo bukta analikunja utafikiri chokoraa,it is a shame

    ReplyDelete
  13. Kinachofanywa na TFF ni unyanyasaji mkubwa wa Tim zingine, wanaacha kuangalia mambo ya msingi wanakaa kuangalia mtu kavaa hvi kesho atavaa hvi, uongozi siyo kwa style hyo, angalia mambo yanayoweza kuifikisha soka la Tanzania katika level nyingine, sio kujenga uhasama na team nyingine, UTAFELII Ndugu.

    ReplyDelete
  14. Karia hajitambui ,naye sijui mkewe akimwambia kaseme hivi Leo kwenye public anashindwa kutumia akili

    ReplyDelete
  15. Ameshafeli huyu, harudi hapo uchaguzi ujao.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic