July 9, 2017⁠⁠⁠⁠⁠Kiungo Gwiji wa Everton, Leon Osman leo ameweka  shada la maua hivi punde kwenye Makaburi ya Jumuiya ya Madola yaliyopo Makumbusho Dar es Salaam.

Katika makaburi hayo wamezikwa wapiganaji wa Vita ya I na ya II ya Dunia.

Osman ambaye amestaafu msimu uliopita kukipuga Everton yuko nchini kwa maandalizi ya mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Everton dhidi ya Gor Mahia itakayopigwa Alhamisi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Osman alicheza mechi 400 akiwa na Everton hadi alipostaafu.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV