July 9, 2017

 
USIKU wa kuamkia leo ilikuwa ni shangwe kwenye Ukumbi wa Mlimani City wakati wa sherehe ya Rapper nguli wa Bongo ambaye pia ni Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Profesa Jay’ aliyefunga ndoa jana hiyohiyo Julai 8, 2017  na mpenzi wake Grace katika Kanisa la St. Joseph lililopo Posta ya Zamani Dar. Katika kusherehekea harusi hiyo, wakati wa kuingia ukumbini Prof. Jay aliingia akiimba wimbo wake wa ‘Kamili Gado’ huku akiwa amemshikilia mkewe, Bi. Grace, wimbo ambao uliamsha hisia kwa waalikwa wakiwemo wabunge Mch. Peter Msigwa na Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambao walionekana kucheza kwa nguvu zote kumsapoti mbunge mwenzao.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV