July 15, 2017




MPIRA UMEMALIZIKA 

Dakika ya 97: Mashabiki wamekata tamaa wanatoka uwanjani, baadhi bado wapo.

Dakika ya 96: Stars wanafanya shambulizi kali mara mbili mfululizo lakini hawafaniki kupata bao.

Dakika ya 95: Stars wanapata kona, inapigwa kipa anaipangua.

Dakika ya 94: Presha imekuwa kubwa, Stars wanapambana kutafuta bao.


Dakika ya 93: Stars wanafanya mabadiliko, anatoka John Bocco anaingia Stamil Mbonde.

Mwamuzi anaonyesha dakika 8 za nyongeza.

Dakika ya 90: Mchezo unaendelea.

Dakika ya 89: Kuna mchezaji wa Rwanda yuko chini, ameumia, machela imeingia kumbeba amekataa, anachechemea kutoka nje ya uwanja. Mchezo umesimama kwa muda.

Dakika ya 86: Rwanda wanapiga shuti kali linaokolewa na Manula inakuwa kona, inapigwa lakini inaokolewa.


Dakika ya 85: Stars wanapata faulo nje kidogo ya eneo la 18 la Rwanda, inapigwa na Bocco kipa anapanguwa inakuwa kona.
Dakika ya 83: Rwanda wanafanya shambulizi la kushtukiza lakini wanadhibitiwa, Stars wanatengeneza mashambulizi kwa kutumia pande zote,
Dakika ya 82: Mchezo umekuwa na matumizi mengi ya nguvu.
Dakika ya 80: Taifa Stars wanafika langoni mwa Rwanda lakini mpira unatoka nje.
Dakika ya 76: Kasi inaongezeka, timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Dakika ya 74: Rwanda wanapata kona, inapigwa lakini inaokolewa.

Dakika ya 72: Mchezaji wa Rwanda anapata kadi ya njano kwa kuchelewesha muda

Dakika ya 64: Mchezo unaendelea.
Dakika ya 63: Mchezaji wa Rwanda yupo chini ameumia, mchezo umesimama kwa dakika mbili sasa, kuna vita nikuvute ya wachezaji wakitaka atolewe nje.

Dakika ya 56: Himid amerejea, mchezo unaendelea.
Dakika ya 55: Madaktari wanaingia uwanjani kumtibu Mao, wanamtoa nje, mwamuzi hatoi kadi yoyote kwa kuwa hakuona tukio.
Dakika ya 54: Gimid Mao yupo chini, amechezewa faulo, kunatokea mvutano baina ya wachezaji wa pande zote.
Dakika ya 53: Rwanda wameongeza kasi, ushindani umekuwa mkubwa.
Baada ya mvutano ikawa faulo, Rwanda wanapiga faulo inapaa juu ya lango.
Dakika ya 50: Kunatokea mvutano, mpira umemgonga mkononi Simon Msuva, mwamwamuzi wa kati akasema faulo, mwamuzi wa pembeni akasema ni penalti.

Dakika ya 46: Rwanda wanafika langoni mwa Stars lakini mpira unatoka.
Dakika ya 46: Rwanda wanafika langoni mwa Stars lakini mpira unatoka.
Kipindi cha pili kimenza.

MAPUMZIKO

MAPUMZIKO
Dakika ya 45 + 2: Mwamuzi anapuliza filimi kukamilisha kipindi cha kwanza, matokeo ni 1-1.

John Bocco na Kichuya wanafanya shambulizi kali langoni mwa Rwanda, lakini shuti la Kichuya linamgonga beki na kurejea uwanjani.


Zimeongezwa dakika mbili.

Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anasimama kuelekea kuonyesha dakika za nyongeza.


Dakika ya 42: Kuna mchezaji wa Rwanda yupo chini, mchezo umesimama kwa muda.


Dakika ya 40: Rwanda wanafanya kazi kubwa kurejea mchezoni baada ya kufungwa bao.


Matokeo ni 1-1, mchezo unaendelea kwa kasi


Dakika ya 34: Himid Mao anafunga kwa penalti.


GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO


Dakika ya 33: Beki wa Rwanda anafanya faulo ndani ya 18 na mwamuzi anaamuru iwe penalti.


Dakika ya 30: Stars wanalishambulia lango la Rwanda.


Dakika ya 25: Stars wanacheza kwa presha, wanatafuta bao la kusawazisha.


Dakika ya 20: Kunatokea mvutano baina ya wachezaji wa Stars na Rwanda baada ya mchezo mmoja wa Stars kuchezewa faulo kisha nahodha wa Stars, Himid Mao akaingilia kati, mwamuzi amewaamua.


Dakika ta 18: Rwanda wanapata bao la kwanza. Walinzi wa Stars walifanya uzembe wakati wa kuokoa mpira uliopigwa kutoka upande wa kushoto mwa uwanja, mfungaji akaumalizia wavuni akiwa karibu na lango la Stars.


GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!


Dakika ya 15: kapombe analia akiwa chini, wenzake wanambembeleza, wanaingia watu wa huduma ya kwanza wanamtoa huku akiwa analia na kujifunika kw ajezi yake.


Dakika ya 15: Kapombe analala chini mwenyewe anaonyesha faulo aliyochezewa ilikuwa na madhara makubwa kwake.


Dakika ya 14: Shomari Kapombe anachezewa faulo, inakuwa faulo kuelekea kwa Rwanda.


Dakika ya 10: Taifa Stars wanatengeneza mashambulizi mara kadhaa lakini walinzi wa Rwanda wapo makini.


Dakika ya 5: Kasi ya mchezo inaongezeka, Stars wanaanza kutengeneza mashambulizi, mashabiki wanashangilia kwa nguvu kuwapa moyo wachezaji wa Stars.


Dakika ya 1: Mchezo umeanza taratibu.


Mchezo umeanza


Timu zinaingia uwanjani, muda wowote kuanzia sasa mchezi utaanza.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic